Posts

Showing posts from July 26, 2021

𝑷𝒓𝒇.𝑳𝒊𝒑𝒖𝒎𝒃𝒂

Image
 Kukamatwa Mbowe: Prof. Lipumba “Rais Samia Hatokwepa Lawama” UdakuspeciallyJul 27, 2021 Prof. Ibrahim Lipumba MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, hawezi kukwepa lawama kufuatia tukio la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo leo tarehe 23 Julai 2021, siku mbili baada ya Mbowe kukamatwa akiwa hotelini jijini Mwanza, akijiandaa kushiriki kongamano la kudai katiba mpya, lililoandaliwa na Chadema. Mbowe alikamatwa na wenzake 11, katika Hoteli ya Kingdom jijini Mwanza, usiku wa kuamkia tarehe 21 Julai 2021, kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali, kufuatia hatua yao ya kuandaa kongamano hilo. “Tunatahadharisha kwamba, vitendo hivi visipodhibitiwa mapema vinaweza kuleta shida na Rais Samia hatokwepa lawama,” “Kwa kuwa mikutano ya hadhara na makongamano ambayo Serikali anayoiongoza inavizuia, vimeruhusiwa na katiba na sheria zin

Askofu Joseph Gwajima Apinga Chanjo Ya Coronavirus

Image
KUMEKUCHA : Chanjo ya Corona Yamponza Gwajima Apingwa Kila Kona ShangaziJul 26, 2021 Ikiwa imepita siku moja baada ya mbunge wa jimbo la kawe Askofu Josephat Gwajima kudai kuwa walioeta chanjo ya virusi vya corona wamelipwa na watu wa nje kuwaangamiza watanzania amepata upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya viongozi nchini Mbunge wa Bumbuli kupitia chama cha mapinduzi (CCM) amesema kuwa kitendo cha mbunge mwezake kupotosha umma juu ya serikali iliyoleta chanjo hiyo kuwa na lengo la kuwadhuru wananchi wake sio sahihi “Kauli ya Askofu Gwajima kuhusu chanjo na dhamira ya Serikali kuleta chanjo nchini haikubaliki. Ni hatari kupotosha watu wanaotuamini kuhusu mambo ambayo hatuna utaalam nayo. Mjadala kuhusu usalama wa chanjo ni sahihi lakini kiapo kwamba Serikali imeileta kuwadhuru watu si sahihi” amesema Makamba. Kwa upande mwingine Mwenyekiti Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dkt.Fredrick Shoo amewaonya viongozi wa dini wanaopinga chanjo ya corona na kuacha kuhusisha chanjo hiyo na mpang