Posts

Showing posts from August 19, 2021

Millard Ayo Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Ajali ya Gari ya Wafanyakazi Wake iliyochukua Uhai wa Wawili

Image
 Millard Ayo Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Ajali ya Gari ya Wafanyakazi Wake iliyochukua Uhai wa Wawili Udaku SpecialAug 19, 2021 Leo imekua siku ngumu sana kwangu na AyoTV Team…. tumeondokewa na Marafiki zetu wawili na mmoja ni Mfanyakazi mwenzetu Mpiga picha wa AyoTV Kanda ya Ziwa Nellyson Grigery (alievaa shati la kijani) na mwingine ni Rafiki yetu Mujitaba Yusuf (hayupo kwenye picha) waliekua wakisafiri pamoja kutoka Mwanza kuja Dar, wamepata ajali Kibaha wakiwa watatu tunamshukuru Mungu Mtu tatu ambae ni Khamis Abdallah Mwandishi wa AyoTV Kanda ya Ziwa @dullahtza (alievaa t-shirt nyekundu) amejeruhiwa na sasa anaendelea vizuri. Daima tutawakumbuka Ndugu zetu hawa, daima tutamkumbuka Nellyson kama Kijana Mchapakazi, humble sana, mwenye kujituma na mwenye nidhamu kubwa sana ya kazi na hata nje ya kazi….. A VERY SAD DAY yani, Nelly alianza kazi hapa TZA (AyoTV) miezi michache tu iliyopita lakini alileta utofauti mkubwa na mchango wake unaonekana, kazi yake ya mwisho kuchukua p
Image
  Mwananchi Habari Zaidi Kitaifa Ongezeko kodi ya majengo kupitia luku kuanza kesho THURSDAY AUGUST 19 2021           Summary Wakati ulipaji wa kodi ya majengo kupitia manunuzi ya luku ukianza kesho, Ijumaa Agosti 20, 2021 kumekuwa na ongezeko la kodi hiyo kwa viwango tofauti.    ADVERTISEMENT By Aurea Simtowe More by this Author Dar es Salaam.   Wakati ulipaji wa kodi ya majengo kupitia manunuzi ya luku ukianza kesho, Ijumaa Agosti 20, 2021 kumekuwa na ongezeko la kodi hiyo kwa viwango tofauti. Hiyo ikiwa na maana kuwa sasa walio na nyumba za kawaida ndani ya kiwanja kimoja watalipa Sh12, 000 kutoka Sh10, 000 iliyokuwa ikitozwa awali na Sh60, 000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka Sh50, 000. Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya na Miji Midogo wao pia wataguswa na ongezeko hilo licha ya wao kuwa na ahueni kwani watalipa Sh60, 000 kwa nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Alphayo Kidata leo inaeleza