Mwananchi Habari Zaidi Kitaifa Ongezeko kodi ya majengo kupitia luku kuanza kesho THURSDAY AUGUST 19 2021 Summary Wakati ulipaji wa kodi ya majengo kupitia manunuzi ya luku ukianza kesho, Ijumaa Agosti 20, 2021 kumekuwa na ongezeko la kodi hiyo kwa viwango tofauti. ADVERTISEMENT By Aurea Simtowe More by this Author Dar es Salaam. Wakati ulipaji wa kodi ya majengo kupitia manunuzi ya luku ukianza kesho, Ijumaa Agosti 20, 2021 kumekuwa na ongezeko la kodi hiyo kwa viwango tofauti. Hiyo ikiwa na maana kuwa sasa walio na nyumba za kawaida ndani ya kiwanja kimoja watalipa Sh12, 000 kutoka Sh10, 000 iliyokuwa ikitozwa awali na Sh60, 000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka Sh50, 000. Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya na Miji Midogo wao pia wataguswa na ongezeko hilo licha ya wao kuwa na ahueni kwani watalipa Sh60, 000 kwa nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Alphayo Kidata leo inaeleza
Mwananchi Habari Zaidi Kitaifa Mtaka: Hali si nzuri Dodoma, chukueni tahadhari dhidi ya Covid-19 TUESDAY AUGUST 03 2021 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka Summary Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewataka wakazi wa Dodoma kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona kwa sababu hali si nzuri mkoani humo. ADVERTISEMENT By Sharon Sauwa More by this Author Dodoma . Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewataka wakazi wa Dodoma kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona kwa sababu hali si nzuri mkoani humo. Ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 3, 2021 wakati akizungumza na askari wa usalama wa barabarani na viongozi wa masoko wa mkoa wa Dodoma. Amewataka askari hao, viongozi wa masoko na wafanyabiashara kuhakikisha wanachukua hatua za kujikinga katika maeneo yao kwa kuvaa barakoa na kunawa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono. Pia amewataka askari wa usalama wa barabarani kuhakikisha watu wote wanakaa kwenye viti (level seat) kwenye dalad
Mwananchi Habari Zaidi Kitaifa VIDEO: DC Handeni aonya wanaonyonya maziwa ya wake zao WEDNESDAY AUGUST 11 2021 Mkuu wa wilaya Handeni, Siriel Mchembe Summary Imeelezwa kwamba sababu inayowafanya wanaume hao kunyonya maziwa ya wake zao wanaonyonyesha nyingine zinatokana na imani za kishirikina. ADVERTISEMENT By Rajabu Athumani More by this Author Handeni. Wanawake wanaonyonyesha wilayani Handeni mkoani Tanga, wamemuomba Mkuu wa wilaya hiyo, Siriel Mchembe kuwasaidia kupaza sauti na kukemea wanaume wao kuacha tabia ya kuwanyonya maziwa kwasababu wanawafanya watoto wasipate maziwa ya kutosha. Ombi hilo wamelitoa leo Jumanne Agosti 10, 2021 kwa Mchembe kwenye maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yaliyofanyika katika mji mdogo wa Mkata na kusema ana taarifa kuwa baadhi ya wanaume wamekuwa na tabia hiyo wakihusishwa na imani za kishirikina. "Niwashauri wale wanaume mnaonyonya maziwa ya wake zenu muache,mnatumia chakula cha watoto wenu na hiyo inasababisha mtoto kupata utapia
Comments
Post a Comment