Mwananchi Habari Zaidi Kitaifa Ongezeko kodi ya majengo kupitia luku kuanza kesho THURSDAY AUGUST 19 2021 Summary Wakati ulipaji wa kodi ya majengo kupitia manunuzi ya luku ukianza kesho, Ijumaa Agosti 20, 2021 kumekuwa na ongezeko la kodi hiyo kwa viwango tofauti. ADVERTISEMENT By Aurea Simtowe More by this Author Dar es Salaam. Wakati ulipaji wa kodi ya majengo kupitia manunuzi ya luku ukianza kesho, Ijumaa Agosti 20, 2021 kumekuwa na ongezeko la kodi hiyo kwa viwango tofauti. Hiyo ikiwa na maana kuwa sasa walio na nyumba za kawaida ndani ya kiwanja kimoja watalipa Sh12, 000 kutoka Sh10, 000 iliyokuwa ikitozwa awali na Sh60, 000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka Sh50, 000. Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya na Miji Midogo wao pia wataguswa na ongezeko hilo licha ya wao kuwa na ahueni kwani watalipa Sh60, 000 kwa nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya M...
Comments
Post a Comment