KUMEKUCHA RAis Samia Suluh Hasanii Apigilia Msumali Tozo Za Simu Dofu Media Jul27,2021



                          






                                                  

                                         KUMEKUCHA: Rais Samia Apigilia Msumari Tozo za Simu
BabaJul 27, 2021

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali inatarajia kupokea ripoti ya kamati maalum iliyoundwa baada ya malalamiko ya wananchi juu ya sheria ya tozo za maiamala ya simu kuanza kutumiak rasmi mapema mwezi huu Julai.


Akizungumza Ikulu jijini Dar es salaam, Rais Samia amesema tozo hiyo ilipitishwa kwa nia njema ya kusaidia maendeleo ya maeneo yenye changamoto nchini mbalimbali nchini ikiwemo shida ya maji, na barabara kwa sehemu za vijijini.

“Hili la miamala ya simu za mikononi kutuma na kupokea fedha tulianza mfumo huu mwezi huu lakini kulikuwa na kelele nyingi kwa wananchi, na sisi kwa sababu ni serikali sikivu tulitumia kama wiki moja hivi kukusanya maoni ya wananchi, tunatarajia kupokea maoni ya kamati hii siku ya keshokutwa” amesema Rais Samia

“Makato haya tuliyaweka kwa nia njema tu, nchi yetu sasa hivi wakulima wameamka na kilimo kikubwa lakini wakivuna wanshindwa kuleta mazao yao kutokana na ubovu wa barabara hivyo sehemu kubwa ya pesa hizi zitaenda kwenye kuboresha miundombinu hiyo ili wakulima wafaidi jasho la kazi zao, kwa hivyo tumesikia kilio cha watanzania kuhusu hili ila tozo hizi zipo lakini tutaangalia ambayo haitaumiz watu” ameongeza

Comments

Popular posts from this blog

Mtaka: Hali si nzuri Dodoma, chukueni tahadhari dhidi ya Covid-19

ZaidiKitaifa VIDEO: DC Handeni aonya wanaonyonya maziwa ya wake zao