Skip to main content

ZaidiKitaifa VIDEO: DC Handeni aonya wanaonyonya maziwa ya wake zao

 


VIDEO: DC Handeni aonya wanaonyonya maziwa ya wake zao

WEDNESDAY AUGUST 11 2021
kunyonyeshapic

Mkuu wa wilaya Handeni, Siriel Mchembe

By Rajabu Athumani

Handeni. Wanawake wanaonyonyesha wilayani Handeni mkoani Tanga, wamemuomba Mkuu wa wilaya hiyo, Siriel Mchembe kuwasaidia kupaza sauti na kukemea wanaume wao kuacha tabia ya kuwanyonya maziwa kwasababu wanawafanya watoto wasipate maziwa ya kutosha.

Ombi hilo wamelitoa leo Jumanne Agosti 10, 2021 kwa Mchembe kwenye maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yaliyofanyika katika mji mdogo wa Mkata na kusema ana taarifa kuwa baadhi ya wanaume wamekuwa na tabia hiyo wakihusishwa na imani za kishirikina.

"Niwashauri wale wanaume mnaonyonya maziwa ya wake zenu muache,mnatumia chakula cha watoto wenu na hiyo inasababisha mtoto kupata utapiamlo maana hapati maziwa ya kutosha, la msingi hakikisheni mnashirikiana kwenye malezi haya mambo mengine acheni",amesema Mchembe.

Ofisa lishe halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Julia Charo amesema kuwa hadi Juni 21, mwaka huu watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano waliobainika kuwa na uzito pungufu ni watoto 3,856 sawa na asilimia 14 ya watoto wote waliohudhuria kliniki.

Amesema kwa upande wa watoto waliopata udumavu ni asimilia 34 ya watoto wote waliopelekwa na kuhudumiwa katika kliniki na wajawazito 7519 waliopimwa wingi wa damu 102 walikutwa na upungufu mkali wa damu.

ADVERTISEMENT

Mmoja wa mama aliyejitokeza kwenye maadhimisho hayo Shani Omari amekiri mtoto asiponyonyeshwa kwa muda muafaka anapata homa za mara kwa mara na aisipopewa chakula kingine ndani ya miezi sita hawezi kupata homa hizo.

ADVERTISEMENT

Comments

Popular posts from this blog

Mtaka: Hali si nzuri Dodoma, chukueni tahadhari dhidi ya Covid-19