Kisa Chanjo Gwajima Kufukuzwa CCM? babaJul 31, 2021


            

     

            

Kisa Chanjo Gwajima Kufukuzwa CCM?

babaJul 31, 2021


Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu mbunge wa Kawe (CCM) Askofu Josephat Gwajima kudai kuwa watu waohimiza chanjo ya corona hawana nia njema na watanzania msimamo unapingana na chama chake cha siasa CCM ambacho kimehaidi kuwachukulia hatua kali wanachama wake wote wanaokwenda kinyume na msimamo wa chama.


Katika taarifa iliyotolewa baada ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho imeweka wazi kuwa chama kitachukua hatua kali dhidi ya wafuasi wake wanaopinga uamuzi wa chama hicho.



Kwa mujibu wa katiba ya CCM mwanachama anaweza kufukuzwa uwanachama iwapo atakiua kanuni na taratibu za chama hicho na kukutwa na makosa hayo na kikao cha kamati kuu.


Ikumbukwe kuwa siku kadhaa baada ya Gwajima kutoa kauli hiyo juu ya chanjo ya corona katibu mwenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka alijitokeza hadharani na kumuonya juu ya matamshi yake.



Unadhani CCM inaweza kufukuza uwanachama mbunge huyo kama atakutwa na makosa ya kukiuka katiba ya chama chake.. tuandikie kwenye comment hapo chini..


Comments

Popular posts from this blog

Mtaka: Hali si nzuri Dodoma, chukueni tahadhari dhidi ya Covid-19

ZaidiKitaifa VIDEO: DC Handeni aonya wanaonyonya maziwa ya wake zao