Skip to main content

Teodoro Nguema Obiang Mangue: His son the president who loves Bugatti cars and Michael Jackson

Teodoro Nguema Obiang Mangue: Mwanae rais anayependa magari ya Bugatti na Michael Jackson

Nguema

CHANZO CHA PICHA,AFP

Kwa miaka mafanikio ya Teodoro "Teodorin" Nguema Obiang Mangue yaliwiana na mafanikio ya nchi yake Equatorial Guinea, kama ilivyopanda na kuboreka kama mzalishaji mkubwa wa mafuta katika Kusini mwa jangwa la Sahara

Mtoto wa Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo anafurahia maisha yake ya kifahari huko California na Ufaransa.

Maisha yake hayo mazuri ni tofauti kabisa na maisha ya wananchi wenzake wengi, ambao wanafaidika kwa kiasi kidogo na mapato yatokanayo na mafuta.

Mtindo wake wa maisha na matumizi yake yanatajwa kuhusishwa na ubadhirifu ambapo sasa Teodorin anakabiliwa na hatia ya makosa ya kiuhalifu nchini Ufaransa, vikwazo nchini Uingereza na rekodi mbaya ya rushwa nchini Marekani.

Lakini nchini kwake, Teodoro mwenye umri wa miaka 52 anaendelea kusalia kuwa makamu wa rais, akijiandaa kuchukua urais kumrithi baba yake mwenye umri wa miaka 79.

Vitendo vya ubadhirifu na ulafi

Teodorin aliishi California mwaka 1991 alipojiunga na chuo kikuu cha Malibu.

Akanunua nyumba lakifahari la thamani ya dola $30m huko Malibu na vitu vyake vingine alivyokuwa navyo Marekani ni pamoja na gari la Ferrari na vitu vya thamani vya kumbukumbu ya mwanamuziki Michael Jackson.

Haya yalibainika mwaka 2014 alipoamriwa na mahakama nchini Marekani kusalimisha mali hizo baada ya kubainika zimetokana na matumizi yake ya fedha zinazonuka rushwa.

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,

Magari ya kifahari yaliyomilikiwa na Makamu wa Rais wa Guinea ya KIkweta yaliuzwa kwa mnada nchini Switzerland

"Kufuatia ubadhirifu na ulafi usiokoma, Makamu wa Rais Nguema Obiang bila aibu aliipora serikali na kufunga biashara nchini mwake ili kusaidia maisha yake ya kifahari nje, wakati wananchi wake wengi tu wakiishi kwenye umasikini wa utupwa," alisema mwanasheria mkuu msaidizi wa serikali Jenerali Caldwell.

Fedha zilizotokana na kuuza mali za serikali zilipaswa kutumika kwa faida ya watu wa Guinea ya Ikweta ".

'Hakuna tena maisha ya kifahari'

Mwaka 2016, waendesha mashtaka wa Switzerland walikamata magari yake 11 ya kifahari. Baadhi ya magari hayo; Bugatti, Lamborghinis, Ferraris, Bentleys na Rolls Royce - yaliuzwa kwenye mnada kwa $27m. Kiasi cha $23m kilipaswa kwenda kusaidia miradi ya maendeleo nchini Guinea ya Ikweta.

Baadae mwaka 2017, ilikuwa zamu ya Ufaransa kumbana Teodorin, alikutwa na hatia na mahakama ya ubadhifu wa fedha na kuamuru kukamatwa kwa mali zake nchini humo.

Licha ya kutokuwepo Mahakamani, alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu, faini ya dola milioni 35, na mali zake za kifahari Ufaransa zilikamatwa. Moja ya mali zake zilizokamatwa Paris ilikuwa na thamani ya zaidi ya dola $120m.

Kwa mujibu wa sheria za Ufaransa, utajiri wote huu uliokamatwa unapaswa kugawanywa kwa watu wa Guinea ya Ikweta.

Hukumu hiyo iliungwa mkono na mahakama ya juu ya rufaa nchini humo, iliyokataa rufaa yake ya kudai kwamba hana hatia na hoja zake kwamba mahakama ya Ufaransa haina haki ya kuamua kuhusu mali zake.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Glavu za Michael Jackson, alizovaa kwenye tamasha lake la ‘Bad Tour’ ziliuzwa kwa mnada huko Veverly Hills, California mwaka 2010

"Kwa maamuzi haya... Ufaransa sio tena mahala pa kufujia pesa zilizoibwa na viongozi wa juu kutoka nje na wasaidizi wao," alisema Patrick Lefas kutoka shirika la Transparency International France.

Wiki iliyopita, Uingereza iliongeza pigo lingine kwa Teodorin kwa kumuwekea vikwazo yeye na viongozi wengine kutoka Zimbabwe, Venezuela na Iraq.

Uingereza ilisema mali zake za kumbukumbu ya Michael Jackson ilikuwa ni pamoja na vikinga mkono au glove zenye thamani ya dola $275,000, glove hizo zilivaliwa na mwanamuzi huyo wakati wa uhai wake kwenye ziara ya tamasha lake lililoitwa 'Bad Tour' katika miaka ya 1980s.

Vikwazo hivyo vya Uingereza vinahusisha kukamata mali, kupiga marufu kupitisha fedha kwenye mabenki ya Uingereza na kusafiri kuingia nchini humo.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Dominic Raab alisema vikwazo hivyo vipya vinawalenga watu hao 'waliojipatia fedha na mali kwa gharama wa wananchi".

Onyo kwa wengine

Licha ya kukabiliana na mashitaka nje ya nchi, Teodorin anaendelea kusalia na nafasi yake kwenye siasa za Guinea ya Ikweta. Baba yake ni kiongozi aliyekaa madarakani muda mrefu zaidi Afrika na anaelezwa na mashirika ya haki za binadamu kama mmoja wa madikteta katili Afrika.

"Wakati Rais akiwa mtu muhimu, mtoto wake anafamika zaidi Afrika Magharibi na Afrika ya kati kutokana na kuvivutia sana vyombo vya habari vya kimataifa ", anasema mchambuzi wa Afrika, Paul Melly.

"Hatua zilizochukuliwa na mahakama katika baadhi ya nchi za Ulaya dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyofanywa na familia za marais wa Afrika ni ishara zinazoweza kuzikumba baadhi ya nchii kwa kupoteza uaminifu na kukosa fedha za maendeleo ," aliongeza.

"Lakini masuala haya wala hayazungumwi na kujadiliwa sana katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara ".

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Comments

Popular posts from this blog

Mtaka: Hali si nzuri Dodoma, chukueni tahadhari dhidi ya Covid-19

ZaidiKitaifa VIDEO: DC Handeni aonya wanaonyonya maziwa ya wake zao